Header Ads

Header ADS

Maseneta 100 waapishwa kama Baraza la Mahakama Katika kesi inayomkabili Trump

  Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa Alhamisi kama baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili rais Donald Trump.
  Hakimu mkuu wa mahakama ya juu zaidi John Roberts aliapisha maseneta kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo.

  Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi.
  Kesi hiyo imepangiwa kuanza kusikilizwa Januari 21.
  Hakimu Roberts aliwauliza maseneta, " Je munaapa ya kwamba katika kesi inayomkabili Donald Trump, Rais wa Marekani, ambayo inayongoja kusikilizwa, mtatenda haki bila upendeleo kulingana na katiba, Mungu awasaidie?"
  Wabunge wakajibu "Ndio" kabla ya kila mmoja wao kusaini kitabu walichochukua nacho kiapo. Kiongozi wa waliowengi wa Republican Mitch McConnell, kisha akaahirisha kikao cha kutathmini iwapo Donald Trump ana kesi ya kujibu na kutangaza kwanza kesi hiyo itaanza kusikilizwa Jumanne, 13:00 EST (18:00 GMT).
   Bwana Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia bunge. Hata hivyo amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni madai ya udanganyifu.

No comments

Powered by Blogger.