Header Ads

Header ADS

Meya wa Dar es Salaam Mwita agoma kuondoka Madarakani.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kwa gharama kesi ya Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ya kutaka kusitisha mchakato wa kumuondoa madarakani.
  Hatua hiyo inatokana na Mwita kuwasilisha maombi hayo kupitia Wakili wake Hekima Mwasipu mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega.

 Wakili Mwasipu ameieleza mahakama kwamba miongoni mwa sababu zao ni kwamba anaona kesi hiyo haina maana kuwepo mahakamani kwa sababu hatua za kumng’oa madarakani zilishafanyika.
 Pia muombaji (Mwita) hakupewa nafasi ya kusikilizwa mahakamani, hivyo anaomba kuliondoa shauri hilo bila gharama.
 Hata hivyo, Wakili wa Serikali Rashid Mohammed amedai kuwa hawana pingamizi na maombi hayo ila wanaomba suala la gharama liwepo kwa sababu wamepoteza muda, rasilimali na uandaaji wa majibu kuhusu shauri hilo.
 Katika uamuzi wake Hakimu Mtega amesema “Nakubaliana na maombi ya muombaji (Mwita) ya kuliondoa shauri hili, hivyo naliondoa kwa gharama”.

No comments

Powered by Blogger.