Mkojo waaminika kuwa ni Dawa ya kupunguza uzito.
BABA wa watoto wawili amefichua kwamba hunywa glasi ya mkojo wake mwenyewe kila siku na anausifu kwa kumwezesha kupunguza uzito kwa kilo 50.
Kwa kipindi cha miaka sita iliyopita, Dave Murphy (54) mkazi wa Basildon, Essex nchini Uingereza amekuwa akinywa mkojo wake, anaosema kuwa unahusika si tu kupungua kwa unene wake bali pia kumletea mwonekano wa ujana na siha njema.
Dave, ambaye aliweza kupunguza uzito kutoka kilo 127 hadi kilo 76 kwa tiba hiyo, pia anaamini mkojo unaweza kuwa suluhu ya uhaba wa chakula duniani na kuweza kubana matumizi kwa wanaofuja fedha baa.
Sehemu kubwa ya siku, Dave hutumia pesa kidogo kwa mlo, ambao pia unahusisha chungwa moja na glasi mbili za mkojo wake mwenyewe
Kile anachopenda zaidi ni sehemu ndogo ya chips kutoka duka lililo jirani, ambazo huagiza mara tatu kwa wiki.

Wakati fulani mwaka 2012 kwa kipindi cha siku 30, Dave hakula kitu kingine chochote zaidi ya mkojo wake.
Dave pia hutumia mkojo wake kunawa uso na kuogea na anasisitiza kuwa mkojo ni bidhaa muhimu ya kuzuia hali ya kuzeeka.
Dave anaeleza: “Baada ya kunywa mkojo wangu, nilijihisi kuwa na afya na mkakamavu kuliko nilivyokuwa kabla na nilipunguza uzito wa kilo 50.
“Zaidi ya hayo, sihitaji fedha zaidi ili kuishi kwa sababu ninachotumia ni mkojo niunywao, ambao unanifanya nisiwe na haja ya kula chakula kingi.
“Kama wanadamu, hatupaswi kutumia kiasi kikubwa kama hicho cha chakula. Mkojo unaweza kutusaidia kupunguza kile tunachohitaji kuingiza tumboni – maana ndani yake kuna kila kitu binadamu anachohitaji.
“Watu wengi wanadhani mkojo wakiunywa ni uchafu lakini si hivyo. Kiuhalisia ni msafi kuliko maji.
“Mkojo ni taswira ya kile ambacho mwili wako unahitaji lakini umezidi zaidi kimanufaa.
“Kwa mfano, iwapo una maambukizo kisha mkojo wako utakuwa na silaha za kupambana nazo. Huboresha mfumo wa kinga na hata kuponya pumu iliyonisumbua kwa muda mrefu wa maisha yangu.
“Tiba ya mkojo si kuhusu kuunywa tu, unaweza kuogea na kujipaka. Ni bidhaa inayozuia ngozi kuzeeka – mikunjo na makunyazi yaliyokuwamo ngozini mwangu usoni na kwingineko mwilini imetoweka tangu nilipoanza kutumia mkojo wangu kuogea na kunawia.
“Unawea kuutumia hata kuondoa maumivu au muwasho na kama vile ya macho.
“Mkojo ni tiba kwa kila kitu. Iwapo watu watabadili mtazamo wao kuhusu tiba hii, hakika kisha kila mtu atashuhudia maajabu na manufaa makubwa ya maji haya kutoka mwilini mwetu.”
Dave alianza matumizi ya mkojo Mei 2011 baada ya awali kusita sita kabla ya kuhudhuria mkutano kuhusu tiba ya mkojo.
Tiba ya mkojo inaelezwa kurudi nyuma nyakati za Biblia na nyaraka za kihistoria zinaeleza namna ulivyokuwa ukiponya majeraha yaliyoambukizwa na manufaa yake pia yameandikwa katika riwaya za Kihindi na Kichina.
Mkojo kwa kiasi kikubwa ni msafi, ukiwa na asilimia 95 ya maji na asilimia tano ya virutubisho kama vile protein, vitamini na madini.
Madini hayo ni pamoja na urea, chloride, sodiamu, potassiamu na chuma.
Baada ya kula na mmeng’enyo wa chakula kufanyika, maji pamoja na mabaki yaliyomeng’enywa husafirishwa katika kibofu cha mkojo.
Maji hayo ndiyo husaidia kufanya usafirishaji wa mabaki hayo hadi katika kibofu cha mkojo.
Aidha, wakati wa mchakato wa usagishaji, maini hushughulika na sumu na kuziondoa.
Kisha damu inaenda katika figo, ambako huchujwa tena na vitu visivyohitajika mwilini hukusanywa katika mchanganyiko wa maji ambao hutoka kama mkojo.
Lakini Dk. Rob Hicks alisema: “kwa miaka mingi watu wengi walidai uwapo wa faida za kiafya kwa kunywa mkojo wao, lakini kwa kadiri nijuavyo hakuna ushahidi wa kisayansi kuunga mkono madai hayo.
“Figo ni mfumo fanisi wa uchujaji wa kuondoa taka mwilini na hiyo ni kazi yake ya asili. Binafsi naamini kuna njia nzuri zaidi na isiyoleta kinyaa za kuufanya mwili kuwa na afya ikiwamo kutovuta sigara, kula mlo bora na kutoruhusu msongo wa mawazo.”
Lakini Dave anakumbushia jinsi alivyokuwa na uzito mkubwa huku akiwa na afya mbovu ikiwamo kusumbuliwa na pumu tangu utotoni, kitu ambacho tangu atumie mkojo kimetoweka.
Anaeleza: “Miaka sita iliyopita nilikuwa na uzito mkubwa na mgonjwa sana, nilitumia steroids kuikabili pumu.
Nikiwa nafanya kazi kama mtaalamu wa program za kompyuta katika Jiji la New York, mlo wangu ulitisha. Ungeniona nikila chocolate siku nzima achilia mbali chakula cha mchana na usiku.

“Wakati nilipotania kwa kuzungumzia tiba ya mkojo na wafanyakazi wenzangu wakati wa tamasha moja, kiukweli sikuwa na lengo hilo. Lakini mwishowe tukaamua tujaribu!”
Tangu hao nikaanza kunywa glasi ya mkojo mara mbili kwa siku. Pamoja na kuwa muwazi kuhusu hilo, anakiri awali alisita na kuona kinyaa kunywa mkojo wake mwenyewe kabla ya kuzoea.
Dave anasema tangu hapo akazoea na kuona ni jambo zuri na matokeo ya unywaji mkojo wake ni kupungua uzito, kuwa na siha ya ujana pamoja na maradhi ya pumu kumtoka.
Ukiachana na hilo mkojo mbali ya kuelezwa kuwa na manufaa kiafya, wanayansi na watafiti Uingereza wameshavumbua nguvu za mkojo katika kuzalisha nishati ambayo inaweza kuchaji simu kwa muda wa dakika 25 na pia kumwezesha mteja kutuma ujumbe na kuperuzi intaneti.
Mbali ya hilo hivi karibuni watafiti nchini Ujerumani wamedai kutengeneza pombe kutokana na mkojo.

No comments
Post a Comment