Ndege Aina Ya Boeing-737 Imepata Ajali Na Abiria Zaidi Ya 170 Ndani
Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.
Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.
Serikali ya Ukraine imesema kuwa inafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo.
Ziara ya Rais Volodymyr Zelensky kuelekea Oman ilisitishwa na amerejea mjini Kyiv, taarifa zinasema.
"Pole zangu nyingi kwa ndugu na jamaa wa abiria wote waliokuwa katika ndege hiyo pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo,".
Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani.
Abiria wapatao 168 na wafanyakazi 9 wa ndege hiyo wamedhibitishwa kuepo kwenye ndege hiyo, Waziri mkuu Oleksiy Honcharuk alisema.
"Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameliviambia vyombo vya habari, Reuters imeripoti.
No comments
Post a Comment