Header Ads

Header ADS

Serikali imevunja Bodi ya Chama cha Wakulima Lupembe Mkoani Njombe.

 Bodi ya chama cha ushirika wa wakulima wa chai Lupembe MVYULU kilichopo wilayani Njombe mkoani humo imevunjwa huku viongozi wake wakiagizwa kukamatwa ili kupisha uchunguzi wa ubadhilifu wa mali za ushirika pamoja na kuendelezwa kwa mgogoro wa miaka mingi baina ya ushirika huo na mwekezaji wa kiwanda cha chai cha Igombola.
 Ripoti ya kiwanda cha chai Igombola lupembe iliyosomwa na kaimu meneja wa kiwanda bwana Allen Mbafu imeeleza kuwa, licha ya kufungwa kwa kiwanda hicho kwa takribani miaka nane kutokana na mgogoro mkubwa baina ya Mvyulu lakini wameendelea kujiimarisha na kutoa ajira kwa wakazi wa lupembe.

“Pamoja na amri ya mahakama kuu lakini wenzetu Mvyulu hawajaonyeshwa nia ya kutekeleza agizo ambalo sasa ni majembe action mart kuchukuwa hatua pamoja na fidia pi kuna ghalama zingine za ziada ambazo zimeainishwa kwenye hukumu”ameeleza Allen Mbafu
 Aidha,Andrew Ulungi ni mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Lupembe licha ya kukiri kupata hasara kubwa kutokana na mgogoro wa miaka mingi baina ya kiwanda,lakini anasema bado wanahitaji msaada kutoka serikalini ili kuinua sekta ya zao la chai.
 Awali wakulima wa chai akiwemo Bosi Mbanga na Rehema Malekela wanalalama kwa kuvutana,huku wengine wakivutia Mvyulu na wengine kwa mwekezaji wa kiwanda ikiwa lengo ni kuona zao la chai linapata soko la uhakika.
 “Hakuna Amcos hata moja huko vijijini,walikuwa wanatumia vitu kama vya kwao,viongozi wa Mvyulu msitufanye sisi wajinga,mnatoa vitu humu kiwanadani na wengine tulikuwa tunaona”amesema mmoja wa wakulima wa chai
Pia, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka anasema hatosita kuchukua hatua kwa maelekezo yote ya naibu waziri Bashe kwani sakata hilo limewarudisha nyuma wakulima wa chai Lupembe kwa miaka mingi sasa kutokana na baadhi yao kuendekeza migogoro na kukimbilia mahakamani.
 “Baadhi ya watu wazima hapa mnashindana kwamba hamuoni makosa yenu na watoto wenu na hasa wale mlio wapa dhamana kwenye ushirika,kwenye ushirika huu sipati kigugumizi kusema ni ufisadi mtupu”amesema Ole Sendeka
Hata hivyo Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili naibu waziri Hussein Bashe kwa kutumia spika za gari la polisi kutokana na mvua kubwa kuendelea kunyesha amelazimika kutoa maelekezo mbalimbali ikiwemo kuvunja bodi ya Mvyulu na kutaka mali zote za ushirika zikatafutwe zilipo.
 “Maamuzi ya serikali ni pamoja na muwekezaji aweze kufanya kazi zake kwa wakati na bila matatizo,lakini pia viongozi wa ushirika ambao wametajwa katika ripoti zote tatu wakamatwe na vyombo vya ulinzi waweze kusaidia kuonyesha mali za ushirika zimekwenda wapi”ameeleza waziri Bashe
  Kiwanda cha chai Lupembe kimekuwa kwenye mgogoro na ushirika wa wakulima wa chai kutokana na kila upande kutoridhishwa na mwenendo uliopo na kulazimika kupelekana mahakamani hatua iliyoifanya serikali ya awamu ya tano kuanza kuchukua hatua madhubuti kwa maslahi mapana ya wakulima na wawekezaji wanaowekeza nchini Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.