Header Ads

Header ADS

DC:Bahath Kitundu amepiga marufuku Michezo ya kubahatisha [BONANZA ] Vijijini

  Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu, amepiga marufuku michezo ya kubahatisha (BONANZA)  katika maeneo ya Vijijini na kuagiza waziondoe zote zilizopo.
  Amesema kwa vijijini hakuna sifa ya kuwepo kwa michezo hiyo hivyo waipeleke kwenye kumbi za starehe maeneo ya Mijini.














 Mkuu wa wilaya huyo amechukua maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, kwamba michezo hiyo haisaidii chochote katika maeneo yao zaidi ya kuwapotezea muda vijana Shughuli nyingine za kimaendeleo.
  "Ni kweli hawajakiuka masharti, lakini bado ofisi yangu  inasema hawa watu wa Bonanza wananchi wanawakataa na sijui kama kwenye vijiji vyetu kuna sifa ya kuwekwa mashine hizo, sasa kauli ya mkuu wa wilaya ni kwamba katika halmashauri ya wilaya ya Babati na mkurugenzi ambaye anatoa leseni  anasikia, hakuna mahali ambapo pana kidhi kuweka mashine ya kuchezesha michezo ya kubahatisha, wote watoke waende Mijini ambapo kunastahili" alisema Kitundu.
  Amesema kuwa mchezo huo unasababisha wanafunzi kuwa watoro na wengine kutoroka muda wa masomo.
  Pia,Amesema sanjari ya serikali kutoa leseni katika michezo hiyo lakini wananchi hawaitaki kabisa michezo hiyo.
 Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Babati Hamisi Malinga amemueleza mkuu wa wilaya kuwa atasimamia agizo hilo lifanyiwe kazi katika maeneo yote ya vijijini ikiwa ni pamoja na kusitisha leseni zilizotolewa kwa ajili ya mchezo huo.

No comments

Powered by Blogger.