Header Ads

Header ADS

Jesusi wa CIA ahukumiwa kifo na Mahakama ya Iran.

  Msemaji wa Idara ya Mahakama nchini Iran Bw. Gholam Hossein Esmaili, ameeleza kuwa Mahakama Kuu ya nchi hiyo imemhukumu kifo Raia mmoja wa Iran ambaye ni Jasusi wa Shirika la Upelelezi la Marekani, CIA.
  Hata hivyo, Shirika la habari la Iran Fars limemnukuu Bw. Esmaili akisema kuwa, Amir Rahimpour, ambaye alikuwa mpelelezi wa CIA, alipewa kiasi kikubwa cha pesa ili kutoa baadhi ya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kwa idara ya ujasusi ya Marekani.

  Ameendelea kueleza kuwa watu wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 kila mmoja gerezani kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa ajili ya Marekani.

No comments

Powered by Blogger.