Katibu Chadema Manyoni auawa, mwili waokotwa barabarani
Mwili wa katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Manyoni, Alex Jonas umekutwa eneo la Mwembeni Manyoni leo asubuhi, Februari 26, 2020 barabarani ukiwa na majeraha.
Taarifa zilizotolewa na uongozi wa chama hicho kupitia mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa katibu huyo aliuawa usiku wa jana na mwili wake umekutwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, kichwani na mikononi.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.
“Ni kweli kunatukio la katibu wa Chadema wilaya ya Manyoni kukutwa amefariki dunia leo asubuhi, Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kutoa taarifa kamili” ameiambia Mwananchi
Hadi sasa bado taarifa kamili juu ya tukio hilo kutoka kwa Jeshi la polisi hazijatolewa, Machweo Communication news itakujulisha kila kitakachojiri.
No comments
Post a Comment