Lukuvi amekabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya kigamboni kama alivyo agizwa na Rais.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais John Magufuli wiki iliyopita.
Februari 11, 2020 wakati akizindua ofisi za mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya Kigamboni pamoja na hospitali ya wilaya hiyo, Rais Magufuli alimwagiza Lukuvi kuhamisha umiliki wa ekari hizo kutoka katika wizara yake kwenda kwa manispaa hiyo.
Leo Jumatatu Februari 17, 2020 , Lukuvi akiambatana na katibu mkuu wa wizara hiyo, Mary Makondo wamekabidhi ekari hizo kwa viongozi wa wilaya na manispaa ya Kigamboni akiwamo mkuu wa wilaya hiyo, Sarah Msafiri.
No comments
Post a Comment