Rais Magufuli amtaka Makonda kurejesha fedha za TASAF kama alizitumia
Rais Magufuli amesema katika Uhakiki wa Kaya maskini uliofanyika kuanzia Novemba 2015 hadi Juni 2017 zilithibitika Kaya hewa 73,561 na Kaya 22,034 zilithibitika sio maskini
Amesema anafikiri fedha hizo ni zilizotolewa kwa Kaya ambazo sio maskini zilitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwenda Dodoma huku akiwa sio maskini

Amesisitiza kuwa kama ni kweli Makonda alitumia fedha za TASAF akaenda nazo huko alikokuwa anaeleza na yeye hahusiki kwenye Kaya maskini basi ni lazima azirudishe fedha hizo
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Awali, RC Makonda amesema kuwa yeye ni mnufaikaji wa mfuko huo kwani alipewa fedha na Rais Mstaafu Mkapa ambaye ni mwanzilishi wa mfuko huo kwenda Dodoma kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM

No comments
Post a Comment