Mashambulizi ya anga ya Urusi yaua watu tisa Syria.
Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Urusi katika kijiji chenye wakimbizi wengi kaskazini mwa Syria, yamesababisha mauaji ya watu wapatao tisa.
Shirika linalofuatilia haki za binaadamu nchini Syria, limesema kuwa mashambulizi hayo yalikilenga kijiji cha Abean kilichoko magharibi mwa jimbo la Aleppo. Shirika hilo limesema watoto sita ni miongoni mwa watu waliouawa.

Idadi hiyo inaweza ikaongezeka kwa sababu watu wengine bado wamekwama kwenye kifusi na 20 kati ya waliojeruhiwa wako mahututi. Ibrahim al-Hajj, msemaji wa idara ya uokozi ya White Helmets, amesema wengi wa waliouawa na kujeruhiwa ni wakimbizi wa Syria ambao walikimbia mapigano kutoka Aleppo.
Pia, Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema kuwa vikosi vya serikali ya Syria leo vimekishambulia kituo cha kijeshi cha Uturuki kilichopo Taftanaz, katika jimbo la Idlib na kuwaua wanajeshi watano.

No comments
Post a Comment