Serikali imetaifisha Mali na fedha Zenye thamani ya Tsh.58
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga akionesha moja ya kipande cha madini ya dhahabu yaliyokabidhiwa rasmi kwa serikali leo baada ya kutaifishwa kwa amri ya mahakama huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akishuhudia.
Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Mhe. Biswalo Mganga akizungumza wakati wa kukabidhi kwa Katibu MMkuu wa Wiizara ya Fedha na Mipango Dotto James mali zilizotaifishwa kutokana na kesi zinazohusiana na uhalifu sambamba na fedha zilizolipwa kutokana na kesi za madini zilizopo katika akaunti ya AFR katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zenye thamani ya Tsh Bilioni 58.6 kutoka kushoto ni Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifun
Dotto Biteko wa Wizara ya Madini wa pili kutoka kulia, Dk. Agustine Mahiga wa Katiba na Sheria na Dk. Philip Mpango wa Fedha na Mipango wakionesha madini yaliyorejeshwa kutoka nchini Kenya baada ya kutaifishwa na serikali kwa amri ya Mahakama ya Tanzania kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Mhe. Biswalo Mganga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Mhe. Biswalo Mganga akionesha moja ya kipande cha madini ya dhahabu yaliyokabidhiwa rasmi kwa serikali leo baada ya kutaifishwa kwa amri ya mahakama huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akishuhudia.
SERIKALI kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefanikiwa kupata amri za kutaifisha mali na fedha zinazohusiana na uhalifu sambamba na fedha zilizolipwa kutokana na kesi za madini zilizopo katika akaunti ya AFR katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zenye thamani ya Tsh Bilioni 58.6.
Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari leo Jumatatu (Februari 10, 2020) Jijini Dar es Salaam, wakati wa makabidhiano ya utaifishaji wa mali za uhalifu mali hizo baina ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na DPP na Katibu Mkuu Hazina, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga alizitaja mali hizo ni pamoja na Nyumba, magari, viwanja, mashamba, mbao na jahazi.
Mganga alisema Ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, mbali na fedha hizo, imepata amri ya kutaifisha nyumba 24, magari 65, viwanja 9, mashamba 2, mbao 6894, jahazi 1 iliyotokana na uvuvi haramu kwenye ukanda wa bahari kuu ya Tanzania pamoja na boti moja ya Yohanda iliyohusika katika kuingiza nchini vipodozi vyenye sumu.
‘’Kwa ufupi ukuchukua thamani ya madini na kiasi cha fedha zilizomo kwenye akaunti ya Asset Forfeiture Recovery (AFR) ya BOT unapata Tsh 19,639,782,781.46 ambazo nakabidhi, hivyo ukijumuisha thamani ya madini yote, fedha iliyolipwa kutokana na kesi zinazohusiana na madini pamoja na fedha zilizomo kwenye akaunti ya AFR jumla yake inakuwa Tsh 58,604,375,783.56’’ alisema Biswalo.
Biswalo anasema tangu kuzinduliwa rasmi kwa ofisi hiyo mwezi Agosti mwaka 2018, Ofisi yake imefanikiwa kutaifisha jumla ya kilo 397.937 za dhahabu zenye thamani ya Tsh Bilioni 32.2 zilizokuwa zikitoroshwa nje ya nchi na kuisababishia serikali kukosa mapato, ambapo kati ya hizo, kilo 351.76 za dhahabu zenye thamani ya Tsh Bilioni 29 zimeshakabidhiwa kwa Katibu Mkuu Hazina ambaye ndiye mtunzaji wa mali za Serikali.
‘’Leo hii nakabidhi jumla ya kilo 46.177 za dhahabu zenye thamani ya Tsh Bilioni 3.2, pamoja na hayo tumeendesha kesi na kufanikiwa kupata amri za kutaifisha madini aina ya Almas, Tanzanite, Silver, Amethyst, Rhodolite, Bati, Blue Sapphire, Spinel, Ruby, Tourmaline, Acuamarine, ambapo jumla ya thamani ya madini yote yaliyotaifishwa pamoja na faini zilizolipwa na washitakiwa ni Tsh Bilioni 42.2’’ alieleza Biswalo.
Katika hatua nyingine, Biswalo alisema kufuatia marekebisho ya sheria mbalimbali Na. 11 ya mwaka 2019, Ofisi yake imeendesha kesi katika zoezi la washtakiwa kukiri makosa yao ambapo jumla ya Tsh Bilioni 12.3 zimeshalipwa kama kodi iliyokwepwa, faini na fidia katika akaunti maalum iliyopo Benki Kuu ya Tanzania.
Akifafanua zaidi Biswalo alisema zoezi la urejeshaji wa fedha kwa washitakiwa 341 ambao hawajamaliza kutimiza makubalino linaendelea na makubaliano hayo yanapaswa kutekelezwa kama yalivyosajiliwa kwa amri ya mahakama, ambapo katika madai hayo Serikali inawadai washitakiwa wote kiasi cha Tsh Bilioni 32.
Kwa mujibu wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga alisema wakati umefika kwa Watanzania kunufaika kikamilifu na uwepo na rasilimali zao ikiwemo madini ambayo katika miaka ya nyuma hayakuwa na usimamizi madhubuti, hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa yanaleta manufaa endelevukwa wananchi wake.
Katika upande wake Waziri wa Madini, Dotto Biteko aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria kwa kuwa serikali haitokuwa na msamaha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya utoroshaji wa rasimali madini nje ya nchi kwani yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuinyima nchi mapato.
Pia, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema zoezi la utaifishaji wa mali za uhalifu, ni dalili tosha kuwa Tanzania sio nchi maskini na hivyo hakuna sababu ya Serikali kwenda kukopa nje ya nchi na badala yake itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa raslimali zake zitalindwa kwa nguvu zote.

No comments
Post a Comment