Syria imekomboa eneo la mwisho la barabara kuu kutoka mikononi mwa waasi
Serikali ya Syria na vikosi vya washirika hii leo vimelikomboa eneo la mwisho la barabara moja kuu kutoka mikononi mwa waasi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Kitendo hiki ni baada ya miezi kadhaa ya mashambulizi kwenye ngome ya waasi ya Idlib na ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 2012 ambapo serikali imeidhibiti barabara nzima ya M5, ambayo inaunganisha mji mkuu Damascus na miji mingine muhimu kama vile Hama, Homs na Aleppo.
Mkuu wa Shirika linalofuatilia Haki za Binaadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman amesema serikali imelikomboa eneo la Rashideen al-Rabea katika mkoa wa Aleppo.
Hata hivyo,Utawala wa Rais Bashar al-Assad ulipoteza maeneo makubwa ya nchi hiyo kwa waasi kutokana na mzozo huo uliozuka kufuatia maandamano ya kuipinga serikali mwaka wa 2011.

No comments
Post a Comment