Mbunge wa Tandahimba Katan Ahmed [CUF] ahamia Chama tawala CCM.
Mbunge wa Tandahimba Mkoani Mtwara (CUF) Katani Ahmed Katani amejiuzulu Ubunge wake na kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano uliofanyika Nanyamba leo Feb 21, 2029.
Aidha,Katani amepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally ambaye yupo kwenye ziara Mkoani humo.
Hata hivyo,Huu ni mwendelezo wa viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani kutangaza kuhamia CCM wakieleza kuwa ni kutaka kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.
No comments
Post a Comment