Header Ads

Header ADS

Wananchi wa Uganda wafanya Nzige kama Kitoweo.

  Raia wa Uganda wanaoishi kaskazini mwa wilaya ya Kitgum wanakula nzige wa jangwani ambao wameharibu mimea yao kulingana na kituo cha habari cha Uganda radio Network URN.
  Hatua hiyo inajiri baada ya ripoti nyingine kwamba raia wa Somali pia wamekuwa wakibadilisha janga hilo la uvamizi wa nzige na kuwafanya kitowe wadudu hao


  Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinasema kwamba raia wa mji wa Adado katikati mwa Somalia wamekuwa wakiwakamata wadudu hao na kuwafanya kitoweo.
  Raia mmoja amesema kwamba wadudu hao ni watamu kushinda samaki,Mwingine amesema kwamba anaamini kwamba wadudu hao wana manufaa ya kimatibabu na kwamba anawafanya kitoweo kwa matumaini ya kupunguza uchungu uliopo mgongoni mwake pamoja na shinikizo la damu,Lakini pia baadhi ya wakazi wameitaka migahawa kuanzisha chakula cha nzige hao.
  Hata hivyo,Uvamizi wa nzige hao katika baadhi ya maeneo nchini Somalia na Ethiopia umeharibu mimea na kutishia bara la njaa katika eneo hilo kulingana na shirika la chakula duniani FAO.

No comments

Powered by Blogger.