Mbwana Samatta kuwasha moto tena leo Ligi kuu England.
MBWANA Samatta mshambuliaji wa Aston Villa, Mtanzania anatarajia kukiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton Uwanja wa St Mary's.
Villa inashuka kwenye mchezo huo wakiwa ugenini jambo litakaloongeza ushindani.
Mchezo wao uliopita walipoteza usiku kwa kufungwa mabao 3-2 na Spurs ya Jose Mourinho.
Huu utakuwa mchezo wa tatu kwa Samatta katika Ligi Kuu ya England tangu ajiunge na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne na nusu akitokea Klabu ya Genk.
Villa ipo nafasi ya 17 ina pointi 25 baada ya kucheza mechi 26 inaparanganyika kujiokoa kushuka daraja.
No comments
Post a Comment