Waziri mkuu wa Lesotho akimbilia nje ya Taifa hilo.
Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane anayekabiliwa na mashitaka ya kumuua mke wake wa kwanza Lipolelo Thabane hakufika mahakamani, wakati alitakiwa kufika mahakamani jana Ijumaa kusikiliza tuhuma zinazomkabili.
Mkewe wa kwanza bwana Thabane,58. alipigwa risasi katika mji mkuu wa Maseru, siku mbili kabla ya bwana Thabane kuwa waziri mkuu 2017.
Mkewe wa kwanza bwana Thabane,58. alipigwa risasi katika mji mkuu wa Maseru, siku mbili kabla ya bwana Thabane kuwa waziri mkuu 2017.
Hakufika mahakamani, alienda Afrika kusini kwa matibabu , na vipimo hivyo ni vya mara kwa mara" , katibu wake Thabo Thakalekoala ameliambia shirika lahabari la AFP.
Wakati huo huo naibu kamishna wa polisi Paseka Mokete amewaambia waandishi wa habari kwamba watasubiri ili kuendelea na kesi hiyo hadi atakaporudi nchini.
“Hatuwezi kwa sasa kusema kwamba alikiuka agizo la mahakama, ” Paseka Mokete ameongeza.
Mapema mwezi Februari 2020, mke mpya wa Waziri Mkuu, Maesaiah, alishtakiwa rasmi kwa mauaji ya mke mwenza na sasa yuko nje kwa dhamana ya dola 67.
Pia ameshtakiwa na jaribio la mauaji ya rafikiye Thato Sibolla ambaye alikuwa na Lipoleo wakati wa tukio hilo la mauaji na anatarajiwa kuwa shahidi mkuu katika mauaji hayo.
No comments
Post a Comment