Header Ads

Header ADS

Serikali ya Tanzania yatanua soko la madini ya bati kimataifa.

  Waziri wa Madini Dotto Biteko  amesema kuwa cheti cha kuuza na kusafirisha madini ya bati nje ya nchi kitatolewa kesho na kueleza kuwa cheti hicho ni hatua kubwa kwa wachimbaji wa madini nchini katika kukuza na kuimarisha sekta hiyo muhimu.
  Akizungumza na wawekezaji katika sekta ya madini katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo jijini Dar es Salaam Biteko amesema Serikali ipo pamoja na wachimbaji hao hasa kwa kushirikiana nao ili kuendeleza sekta hiyo adhimu.

  "Mkutano huu ni wa kutangaza fursa na kubwa zaidi ni kesho ambapo tutapokea cheti cha kusafirisha madini ya bati nje ya nchi kibali ambacho hatukuwa nacho awali" ameeleza Biteko.
  Lakini pia amesema mafanikio katika sekta hiyo ni makubwa na yenye tija kwa taifa kwani hata ukusanyaji mapato kwa sasa mapato yanayokusanywa yamefikia zaidi ya shilingi bilioni 300.
  Awali akizungumza wakati wa warsha hiyo Mwenyekiti wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini  Tanzania (FEMATA) John Bina ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya madini kwa kuonesha ushirikiano hasa katika utatuzi wa changamoto.
  " Changamoto zilizokuwa zinatukabili zimetatuliwa kwa asilimia 80 na tunafurahi kwa sasa Sheria ya madini ni faaafu na Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji" Ameeleza Bina
   Pia amewataka wachimbaji hao kushirikiana katika kuendeleza sekta hiyo na kueleza kuwa ikitokea kukawa na siku ya madini, wachimbaji wamependekeza siku hiyo iitwe "Magufuli Minerals Day" na hiyo ni kutokana na mchango mkubwa wa Rais Magufuli katika kuinua na kuweka mazingira bora kwa ukuaji wa sekta hiyo.
   Mkutano huo wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwa mwaka 2020 uliobeba kauli mbiu ya "Uwekezaji na Ushiriki katika sekta ya madini" umehudhuriwa na mawaziri wa madini kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Uganda na Congo na utafungwa kesho na waziri Mkuu Kassim  Majaliwa.

  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifurahia hotuba ya Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko wakati alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na  nje ya nchi.

No comments

Powered by Blogger.