Mpiga Kinanda wa Kanisa la Kilutheri ambaka Mtoto wa Darasa la Sita.
Polisi mkoani Manyara linamtafuta kijana aliefahamika kwa jina la Elibariki Naeli kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka kumi mwanafunzi wa shule ya msingi Sora katika kitongojiji cha Kansi, kijiji cha Mwinkatsi, wilayani Babati.
Inaelezwa kuwa Kijana anaedaiwa kufanya kitendo hicho cha kikatili anakadiriwa kuwa na umri kati ya 20- 25 ni mwimbaji wa kwaya na mpiga kinanda katika kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania eneo la Kansi mtaa wa Mamire.
Pia,Mama wa mtoto huyo, Christina Gwandu anaemuuguza mtoto wake amesema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 4,2020 majira ya saa 12:30 jioni wakati mtoto huyo akitoka kwa bibi yake alipokuwa amemuagiza kupeleka mboga, ndipo mtuhumiwa akamkamata kisha kumwingiza kwenye kichaka kilichopo jirani na kanisa la KKKT Kansi na kumbaka huku akimtishia kumuua kama angepiga kelele.
Baada ya kumaliza haja yake,mtuhumiwa alimtelekeza kichakani hapo kwa sharti la kutopiga kelele ambako mtoto huyo alijikokota hadi nyumbani.
“Ilibidi nifanye haraka kumpelekea zahanati ya kijiji cha Mwinkatsi ndipo daktari akabainisha kuwa ni kweli amebakwa na kupata maumivu makali” alisema Mama wa mtoto huo.
Akisimulia kisa hicho mtoto huyo anaesoma darasa la tatu katika shule ya msingi Sora, anasema wakati akiwa njiani kurudi kwa bibi alikutana na kijana huyo akiwa na Laiti lakini baada ya kupishana alimuaga yule Laiti na kurudi akikimbia, na alipomfikia alimshika mkono kwa nfuvu kisha kumbeba begani huku akiwa amemziba mdomo asiweze kutroa sauti.
Anaendelea kusimulia “Nilimwambia niachie kwani nimekukosea nini? Akanitishia kuwa nikisema tu atanichinja”
Kwa maelezo ya jirani Rehema Handa,amesema alimuona mtoto huyo akitembea kwa shida ndipo alipoamua kumuangalia na kugundua nguo zake zimeloa damu, na alipomuuliza alimweleza kuwa amefanyiwa kitu kibaya na kijana aliemtaja kwa jina la Elibariki Naeli.
Ameeleza kuwa alimwambia mama wa mtoto hali hiyo ambaye naye aliwahi kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji ingawa hawakufanikiwa kumpata mtuhumiwa huyo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kitongoji hicho , Jeremiah Burra amekiri kutokea tukio hilo ambapo amesema aliwakusanya vijana na kuanza kumtafuta mtuhumiwa huyo bila mafanikio na kwa sasa zoezi la kumsaka linaendelea.
Kwa mujibu wa daktari mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kuwa walimpokea mtoto huyo akiwa katika hali mbaya na walipompima walibaini kuwa amefanyiwa kitendo hicho.
No comments
Post a Comment