Header Ads

Header ADS

Wakazi wa mtaa wa Londoni uliopo kata ya Lizaboni manispaa ya Songea wameitaka Serikali kuwajengea kivuko kinachounganisha Eneo Hilo na TFS Ruhuwiko.

Wakizungumza wananchi wa eneo Hilo wamesema kutokana na kivuko hicho kuwa kibovu wanashindwa kufanya biashara hususani wale wanaotegemea shughuli zao za kiuchumi kufanyika eneo la Ruhuwiko hususani katika kipindi hiki cha masika
  Vilevile,wameeleza kuwa pindi inaponyesha mvua kubwa hata wanafunzi wanashindwa kutumia kivuko hicho hali ambayo inapelekea kupungua kwa wanafunzi au kuwepo kwa maudhurio duni ya wanafunzi katika masomo asa kwa wale ambao wanatokea eneo la Ruhuwiko kwenda kusoma shule ya msingi Londoni 












































       Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Odo Mbunda,amesema atafanya mazungumzo na viongozi wake wa chini ikiwemo Wenyeviti wa mtaa na Wajumbe wake ili waweze kuwatangazia wananchi wa eneo Hilo waweze kujitolea kutengeneza kivuko cha muda huku wakisubiri bajeti ya Serikali ili kuweza kujenga kivuko cha kudumu zaidi.
  Aidha,amewataka wananchi wa mtaa huo na wananchi wa Kata kwa ujumla kuiamini Serikali yao huku wakidhidi kuwa wavumilivu ambapo viongozi wanatafuta njia mbadala
   Hata hivo,amewaomba wananchi wa eneo Hilo kushirikiana kwa pamoja katika Kila kazi ya UMMA ili kuweza kuleta maendeleo ya kata yao kwa pamoja lakini pia maendeleo kwa haraka 

                     Imeripotiwa na mwandishi wetu:Adolf Mwingira_ Songea --Ruvuma


No comments

Powered by Blogger.