Mtendaji kata wa kata ya bombambili iliopo Manispaa ya Songea Hassan Omary Mataja amewakutanisha Wazee wa kata hiyo Katika mkutano.
Mtendaji kata wa kata ya bombambili iliopo Manispaa ya Songea Hassan Omary Mataja amewakutanisha Wazee wa kata hiyo Katika mkutano.
Hassan Mataja ambaye ni mtendaji kata amesema amezungumza na wazee hao kwa lengo la kujenga kata yao ikiwemo Wazee Ni moja kati ya watu muhimu Katika kata.
Hata hivyo,amewataka wanufaika wa TASAF kutumia kiasi cha fedha hiyo Katika kufanya mambo mazuri au kuzitumia Katika kuanzisha miradi mbalimbali ili wengene waweze kutambua umuhimu wa Fedha hizo pia pindi wanapopatwa na matatizo mbalimbali ikiwepo kuugua basi ziweze kuwasaidia na pasipo kutumia Katika ulevi pamoja na kuongeza wake.
Vilevile,amewaomba wazee Katika kata hiyo kushiriki Katika masuala ya kuuziana viwanja pamoja na nyumba ili kupunguza migogoro inayotokana na kuuziana viwanja pamoja na nyumba kwa sababu wazee Ni wenye uelewa na sehemu husika au wanayafahamu vyema maeneo yao
Mwisho,amewapongeza wazee wote walioweza kuudhuria Katika kikao hicho hicho na kuwaomba kuendelea kishirikina hata Katika masuala ya ulinzi na usamala Katika maeneo yao
Nimezungumza na mmoja kati ya wazee hao ambaye ni Rijazi Jonasan Chaula kwa niaba ya wazee waliojitokeza Katika kikao hicho amempongeza mtendaj huyo kwa kutambua thamani na uwepo wa wazee Katika kata yao huku awataka kuendelea kuitisha mkutano wa wazee mara kwa mara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Katika kata hiyo amesema wao Kama wazee amewataka wananchi wanaokwenda vilabuni muda wa kazi kuacha tabia hizo na watachukuliwa hatua za kisheria hususani wale watakaopuuza tamko Hilo huku akiwataka kujikita zaidi kwenye biashara kwa lengo la kujenga kata yao.
Hata hivyo amawataka viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na Wajumbe wao kutambua uwepo wa Baraza huru la Wazee na kuwashirikisha wazee Katika Kila jambo
No comments
Post a Comment