Wafanya biashara wa Nyanya wamelalamikia uhaba wa Nyanya na kupanda kwa bei ya Nyanya Katika Manispaa ya Songea
Wafanya biashara wa Nyanya wamelalamikia uhaba wa Nyanya na kupanda kwa bei ya Nyanya Katika Manispaa ya Songea
Wakizungumza Wafanya biashara wa Nyanya Katika soko la Manzese A Songea wamesema kwa mwaka huu bei ya Nyanya imepanda zaidi ukilinganisha na miaka kadhaa ya nyuma ambapo bei ilikuwa sio kubwa sana lakini kwa sasa licha ya being kuwa kuwa Upatikanaji wa Nyanya umekuwa mgumu
Aidha,wakidai Hilo Ni kutokana na kupungua kwa wakulima kulima Nyanya huku zikiitajika kwa kiasi kikubwa na wafanya biashara kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mtwara na Lindi wakitegemea Nyanya zinazolimwa Mkoani Ruvuma.
Hata hivyo,Wameeleza kwamba Licha ya kubadilika kwa hali ya hewa na Nyanya kuaribika mashambani Bado being ya pembe jeo kwa ajili ya wakulima zimekuwa being ya juu zaidi sababu iliyopelekea wakulima wengi kuachana na kilimo hicho na kufanya shughuli zao zingine
Lakini kwa upande wao wakulima wa Nyanya Katika Manispaa ya Songea wamesema kuwa changamoto inayopelekea kupungua kwa uzalishaji wa kilimo hicho Ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,pindi mvua inyeshapo hali ambayo Nyanya nyingi huaribika ukilinganisha na kilimo cha kiangazi.
Pia,wameiomba Serikali kupunguza gharama ya bei ya pembe jeo ili kuwawezesha wakulima wengi kijikita kuwekeza kwenye kilimo hicho ambapo itapelekea kuongezeka kwa zao Hilo na kupungua kwa bei .
Imeripotiwa na Mwandishi wetu: Adolf Mwingira_Songea - Ruvuma.
No comments
Post a Comment