Odion Ighalo ameeleza kisa cha kupunguzwa mshaara ili atimize ndoto zake.
Mshambuliaji mpya wa Manchester United Odion Ighalo amesema kuwa alikubali kupunguzwa mshahara ili atimize ndoto yake ya kucheza ndani ya Old Trafford.
Ighalo, aliyewahi kuichezea Watford amesema kuwa hakulala wakati anasubiri kusaini mkataba na timu yake mpya, amejiunga kwa mkopo United akitokea Klabu ya Shanghai Shenhua hadi mwisho wa msimu huu.
Hata hivyo, Raia huyo wa Nigeria mwenye miaka 30 amesema kuwa mama yake alilia kwa furaha aliposikia dili la mwanae kutua Manchester United.
No comments
Post a Comment