Marekani imetoa tahadhari juu ya mpango wa Guinea kufanikisha kura ya maoni ya Alpha Conde kusalia madarani.
Marekani imetoa tahadhari kuhusu mpango wa serikali ya Guinea kufanikisha kura ya maoni ambayo, upinzani unasema ni mpango wa Rais Alpha Conde kusalia madarakani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, ambae alimtaka Conde kuheshimu kipindi cha mpito cha kidemokrasia walipokutana mwaka jana, amesema Marekani ina wasiwasi na mpango wa kura ya maoni ya Machi Mosi pamoja na uchaguzi wa bunge
Katika taarifa yake Pompeo amehoji kuhusu uwepo wa mchakato huru, wa haki, uwazi na kuakisi wapiga kura halisi. Aidha kutokana na mashaka hayo ametaka kuwepo kwa majadiliano yatakayoshirikisha pande zote.
Conde mwenye umri wa miaka 81, alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa upinzani nchini Guinea ambae aliingia madarani kufuatia uchaguzi wa 2010, kwa ahadi ya kukabiliana na rushwa.
Baadae alichaguliwa tena 2015. Lakini kwa sasa analalamikiwa kwa utawala wa mkono wa chuma akionekana mwenye kutaka kuvuruga utaritibu wa mihula miwili madarakani.

No comments
Post a Comment