Header Ads

Header ADS

Ugonjwa kifafa kuongezeka mkoani Ruvuma.

Kila februari 10 ya kila mwaka Duniani huadhimisha Siku ya Ugonjwa wa kifafa na kwa mujibu wa shirika la afya Duniani WHO limesema kuwa asilimia 80 ya ugonjwa huo umeenea zaidi katika Nchi zinazoendelea.













Lakini katika Mkoa wa Ruvuma hali imezidi zaidi lakini je,Wananchi wananchi wa mkoa huo wanauelewa na Ugonjwa huo.Nimezungumza na baadhi ya wananchi katika manispaa ya Songea wameonesha kutofahamu sababu za Ugonjwa huo.
Hata hivyo ,Nimekutana na Yona Alfred Mwakabumbe ambaye ni Daktari bingwa wa Tiba katika Hospitali ya Ruvuma ambapo amesema
''Mkoa wa Ruvuma Ugonjwa wa kifafa umezidi kukua au kuenea kwa kasi zaidiambapo kwa mwaka2019 Wagonjwa 16,861 walitibiwakatika Vituovya afya vilivyopo mkoani humo,Huku Wilaya ya Tunduru ikiwa kinara zaidi kwa kuwa na Wagonjwa wengi wakiwa 6355,Songea Mjini zaidi ya Wagonjwa3000,Huku mbinga mjini wakiwa wagonjwa 1900 kwa hiyo namna hii ni wazi Ugojwa huo upo kiasi kikubwa'' ameeleza Daktari Yona.
Aidha,Daktari Yona amesema sababu moja wapo ya kutokea kwa ugonjwa huo ni pamoja na kurithi kutoka kwa Wazazi ,Bibi na hata Babu,Majeraha mbalimbali yanapotokea kwa Mtoto kutokana na kucheleweshwa kwa mama wajawazito wakati wa kujifungua yaani Uzazi Pingamizi,Ajalianazozipata Mtoto wakati wa ukuaji kama vile ajali ya Gari ,Pikipiki na zinginezo. lakini pia Ukosefu wa madini.
Vilevile amewataka Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuchukua Tahadhari kwa Mwathirika wa Ugonjwa Huo kama vile kumsaidia Pindi tatizo linapotokea kwa Mgojwa huyo,kuepuka kumwekea vitu vigumu mdomoni kama Kijiko,Akina mama wakati wakujifungu wafikishwe kwenye vituo vya Afya kwaajili ya Usalama zaidi,Lakini kuondokana na imani za Kishirikina yaani Imani potofu'

               Imeripotiwa na Adolfu Mwingira - Songea -Ruvuma
 







No comments

Powered by Blogger.