Header Ads

Header ADS

Wahariri wa vyombo vya habari watakiwa kutumia lugha kwa ufasaha

       Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mohamoud Thabit Kombo  amewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuitumia lugha ya Kiswahili fasaha kwa lengo la kufahamika na jamii.
Hayo aliyasema huko katika Ukumbi wa Wizara ya habari utalii na mambo ya kale Kikwajuni wakati wa             Mkutano wa Wahariri wa Vyombo  vya Habari  vya Zanzibar.
Alisema utumiaji wa lugha ya  Kiswahili fasaha utasaidia muongozo mzuri wa kufahamika na jamii pamoja na kuilinda lugha ya Kiswahili isipotee.



Aidha alisema Wahariri, Waandishi wa Habari pamoja na Watangazaji  ni vyema kuisimamia lugha hiyo ili iweze kurekebisha mapungufu yanayojitokeza katika matamshi .

Alifahamisha kuwa katika kuikuza lugha ya Kiswahili sanifu ili itumike kama inavyohitajika Baraza la Kiswahili (BAKIZA) wameweza kusambaza makamusi katika vituo vya Habari nchini.

Waziri huyo alisema baada ya mafunzo hayo anatarajia mabadiliko makubwa katika utumiaji wa lugha ya Kiswahili fasaha kwa Watangazaji wa Vyombo vya Habari ikiwemo Radio  Televisheni pamoja na Magazeti.

Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili (BAKIZA) Dkt Mwanahija Ali Juma alisema tafiti mbali mbali zimeshafanywa na baraza hilo na kuweza  kuona makosa ya Kiswahili sanifu yaliyofanyika katika  magazeti mbali mbali ikiwemo na gazeti la Serikali  la  Zanzibar leo.

Alisema kuwa wameweza kugundua makosa mengi yakiwemo udondoshaji  wa viambishi katika vichwa vya habari ,  vitenzi kudondosha wakati jambo ambalo linachangia mkanganyiko kwa msomaji wa gazeti hilo

Alisema kuna makosa ya kijumla kwa upande wa viambishi hata katika matini vipashio katika uwambishaji wa maneno,tahajia pamoja na utaratibu wa uundaji wa maneno .

Alielezea kuwa Kiswahili kimesanifiwa kuwa  lugha ya Kiswahili sanifu na lahaja zipo kwa lengo la  kuusaidia uhai wa lugha hiyo kwa kuengeza misamiati.

Akizungumzia kwa upande wa Radio jamii alisema Watangazaji hawajakatazwa kutumia lugha zao kupitia katika vituo vya jamii kwa lengo la mafahamiano ya lugha  na jamii  husika,  sio kwa radio za kitaifa ambazo zinawasikilizaji wengi.

Nae Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar  Omar Said Ameir  alisema katika kuimarisha na kujenga upendo na wahariri, watayarishaji vipindi pamoja na watangazaji wameandaa mashindano ya matumizi ya  lugha sahihi ya Kiswahili sanifu kwa vyombo mbali mbali vya habari, kukusanya vipindi vyao vilivyoanzia Januari mosi hadi Januari 31 mwaka 2020  vitakavyoshinda vitapatiwa  tunzo maalum  ya ushindi huo .

Mkutano wa siku moja wa  Wahariri wa  Vyombo mbali mbali umetayarishwa na  Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments

Powered by Blogger.