Header Ads

Header ADS

RC Ole Sendeka ashauri kutungwa sheria za kuvutia wawekezaji

          Ili kukuza uchumi na ustawi wa nchi na wananchi wake kwa ujumla, mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameshauri na kukumbusha mihimili mitatu ya serikali hususani bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kutunga sheria rafiki na zitakazowavutia wawekezaji kuwekeza na kutoa mchango kwa uchumi wa Tanzania.Ole Sendeka amesema uchumi unachochewa kati ya sekta ya umma na sekta binafsi hivyo ni jukumu la mhimili wa utendaji yaani serikali,bunge pamoja na mahakama kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji.

 
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameyasema hayo hii leo akiwa mgeni mahususi katika maadhimisho ya wiki ya sheria kimkoa kuelekea kilele cha siku ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe mkoani hapo.

“Sekta binafsi huko ndiko waliko wawekezaji wa ndani na wa nje kwa hiyo ni jukumu la mhimili wa utendaji kwa maana ya muhimili wa serikali,ni jukumu la mhimili wa mahakama,ni jukumu la mhimili wa bunge kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji”alisema Ole Sendeka

Aidha Ole Sendeka ameendelea kuwakumbusha majaji na mahakimu kutoa kipaumbele katika kusikiliza mashauri yanayohusu uchumi kutokana na maelekezo ya viongozi wa juu wa mhimili wa mahakama.

“Na mimi Naomba niyaazime maneno machache ambayo yalikuwa ni maelekezo ya viongozi wa juu wa mhimili wa mahakama kuelekeza na kuwashauri majaji na mahakimu kutoa kipaumbele katika kusikiliza na usikilizaji wa mashauri yanayohusu uchumi,mabenki,viwanda,ushirika,migogoro ya ardhi,rushwa,uvuvi halamu na kadhalika ambayo yametolewa na aliyekuwa jaji kiongozi Manento kupitia waraka wake namba moja mwaka 2007”alisema Ole Sendeka.

Innocent Kibadu ni katibu wa chama cha mawakili wa kujitegemea Tanzania TLS kanda ya Iringa,amesema chama cha mawikili kimeendelea kushirikiana na mahakama kutoa elimu na msaada wa sheria kwa wananchi katika maswala mbali mbali ikiwemo miradhi,ukatili wa aina mbali mbali  kwa kuwa ni baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa na migogoro mingi katika jamii.

Hata hivyo amesema chama cha mawakili wa kujitegemea kinatoa rai kwa mahakama kwenda mbele zaidi kutengua vipengele vya sheria kwa njia ya hukumu na kutoa mapendekezo na mabadiliko kwa sheria zinazoweza kuathiri usalama na imani kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Naye Seif Ahmed ambaye ni mkuu wa mashataka na wakili wa serikali mkoa wa Njombe amesema upo wajibu mkubwa kwa wadau waliopo katika mfumo wa sheria,kuhakikisha unatengenezwa mfumo mzuri wa sheria ili kuweka mazingira salama kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

“Kama wadau ambao tupo kwenye mfumo wa sheria tunaowajibu mkubwa kuhakikisha tunatengezeza mfumo mzuri wa sheria,ili kupiga hatua na kutoa haki kwa wakati kwa mujibu wa sheria ili kuweka mazingira wezeshi na salama kwa wafanyabiashara na wawekezaji alisema” Seif Ahmed.

Baadhi ya wakazi mkoani Njombe walioshiriki katika maadhimisho hayo wameendelea kutoa wito kwa mahakama kuharakisha na kumaliza kwa wakati uendeshaji wa mashauri ili kuepuka ghalama wanazokutana nazo wakati wa kesi zao.

Wiki ya sheria ambayo ni mahususi kwa ajili ya utoaji wa elimu ya sheria na taratibu za kimahakama yanaashiria kuanza rasmi kwa mwaka mpya wa shughuli za  mahakama, yanaambatana na kauli mbiu yenye maudhui “Uwekezaji na biashara:wajibu wa  mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji”

No comments

Powered by Blogger.