Virusi vya Corona: Wasiwasi mkubwa waendelea kutanda ulimwenguni
Wasiwasi unaendelea kuwa mkubwa duniani kuhusiana na mlipuko wa virusi vya corona ambavyo hadi sasa vimesababisha vifo vya watu 563.Hofu zaidi imeendelea kutanda baada ya maelfu ya watu waliomo kwenye meli mbili za kuvinjari kuwekwa kwenye karantini ndani ya meli hizo.
Zaidi ya watu 28,000 wameshaambukizwa nchini China, mnamo wakati maafisa wanajitahidi kuudhibiti mlipuko huo, licha ya kuwalazimisha mamilioni ya watu kusalia ndani ya majumba yao katika miji kadhaa.
Zaidi ya nchi 24 zimethibitisha kuwa na watu walioambukizwa virusi hivyo vilivyoanza mwishoni mwa mwaka jana katika soko linalouza wanyama wa porini.
Maelfu ya watu katika meli mbili za kuvinjari nchini Japan na Hong Kong wanalazimika kusubiri kujua hatima yao, ikiwa baadhi yao wameambukizwa au la. Watu 20 waliomo kwenye meli kwa jina Diamond Princess wamethibitishwa kuambukizwa.
Abiria 3,700 kutoka katika zaidi ya nchi 50 waliomo kwenye meli kwa jina World Dream pia wamewekwa kwenye karantini baada ya watu wanane miongoni mwao kuthibitishwa kuambukizwa.

No comments
Post a Comment