Wanajeshi 33 wa Uturuki Wauawa Katika Mapigano Makali Huko Syria
Wanajeshi 33, wa Uturuki wameuawa katika mapigano kwenye mkoa wa Idlib nchini Syria, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la serikali ya Uturuki, Anadolu, lililomnukuu gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay lililopakana na mkoa wa Idlib, Rahmi Dogan.
Dogan amesema wanajeshi hao wamekufa katika shambulizi la angani lililofanywa na ndege za jeshi la serikali ya Syria na kuongeza kuwa kulikuwa na wanajeshi waliojeruhiwa vibaya sana na wanaendelea kupatiwa matibabu.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amefanya mikutano miwili ya dharura jana jioni kujadiliana kuhusu hali ilivyo katika mkoa huo wa Idlib.
Waziri wa mambo ya kigeni, Mevlut Cavusoglu kwa upande wake alijadiliana kwa njia ya simu na katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami barani Ulaya, NATO Jens Stoltenberg, kuhusu hali kwenye mkoa huo hii pia ikiwa ni kulingana na Anadolu.
No comments
Post a Comment