Header Ads

Header ADS

Kampuni ya Mtandao wa Twita yampa onyo Dolnad Trump

    Katika Chapisho la rais Donald Trump katika mtandao wa Twitter kwa mara ya kwanza limepatiwa onyo na mtandao huo.
Rais Trump alituma ujumbe uliosema: Haiwezekani kwamba makaratasi ya kupigia kura yaliotumwa kwa njia ya posta yanaweza kukosa kufanyiwa udanganyifu.
Twitter iliweka onyo chini ya chapisho hilo na kutuma ujumbe wake kuhusu habari zinazopotosha.
Bwana Trump alijibu kwa kusema kwamba kampuni hiyo ya mtandao inakandamiza uhuru wa kujieleza.
Onyo hilo la Twitter liliandikwa kwa wino wa buluu na alama ya mshangao chini yake, likipendekeza kwamba wasomaji wanapaswa kuangalia ukweli kuhusu makaratasi ya kupigia kura yanayotumwa kupitia huduma ya posta.
Rais wa Marekani Donald Trump. Picha: 26 May 2020
Donald Trump's tweet and Twitter's warning sign below the post

No comments

Powered by Blogger.