Polisi Nchini Marekani wafyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji baada ya kifo cha mtu mweusi
Kumekuwa na vurugu na mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minneapolis nchini Marekani baada ya kifo cha mwanaume mmoja mweusi akiwa mikononi mwa polisi
Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na waandamanaji walirusha mawe na kupulizia mapambo ya graffiti kwenye magari ya polisi.
Kilichotokea kwenye maandamano
Walianza siku ya Jumanne jioni, wakati mamia ya watu walipofika katika eneo ambalo tukio lilitokea, Jumatatu jioni.
Waratibu walijaribu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuzingatia masharti ya kukaa mbalimbali, waandamanaji waliimga ''siwezi kupumua,'' na ''ingeweza kuwa mimi''.
Mmoja wa waandamanaji Anitha Murray aliliambia gazeti la Washinton Post: ''inaogopesha kuwa hapa wakati wa janga la corona, lakini kwa nini nijiweke mbali?''
Kundi la mamia ya watu baadae waliandamana mpaka kwenye idara ya polisi 3rd Precinct, ambapo maafisa waliohusika na kifo hicho walikuwa wakifanya kazi.
Mtu mmoja alikiambia chombo cha habari cha CBS: ''Hii ni mbaya sana. Polisi lazima watambue kuwa hali hii wameitengeneza wenyewe.''
Polisi wamesema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi lakini taarifa za kina hazijatolewa kuhusu tukio hilo.
No comments
Post a Comment