Header Ads

Header ADS

Omar al-Bashir akabiliwa na adhabu ya kifo

Kesi mpya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Sudan Omar al-bashir ilianza jana jumanne julai 21.rais huyo aliondoka madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2019.





















Mnamo mwezi desemba mwaka jana Omar al-bashir alihukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kosa la rushwa.
Mwaka 1989 yalifanyika Mapinduzi ya Omar al-Bashir dhidi ya Sadiq al-mahdi ambaye alikuwa Waziri mkuu wa Sudan kwa wakati huo na kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo ya Sudan.
  Baada ya omar al-bashir kuiongozua Sudan kwa mkono wa chuma kwa miaka 31 sasa anatarajia kujibu tuhuma zinazomkabili mbele ya mahakama maalumu inayoundwa na mkuu wa mahakama kuu na majaji wawili kutoka mahakama ya  rufaa.
  Omar al-Bashir anatuhumiwa kukiuka agizo la katiba na anahukumiwa adhabu ya kifo,pia atahukumiwa na watu wengine 16 raia wa kawaida na askari akiwemo makamu wa Rais Taha na Jeneral Bakri HassanSalehe.
  Pia Mohamed Al Hassan Al Amin mmoja wa wanasheria wa Omar al Bashir amesema kesi dhidi ya mteja wao ni ya kisiasa.

No comments

Powered by Blogger.