Header Ads

Header ADS

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty internationa limesema Tanzaniz inapaswa kutoa ushahidi wa tuhuma zinazo mkabili kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe

 Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty international limesema kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kutoa ushahidi dhidi ya kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani  Tanzania ama wakishindwa kutoa ushahidi basi wamuachie huru .Taarifa ya Amnesty inakuja huku Mbowe akitarajiwa kupandishwa mahakami mapema kesho siku ya alhamisi.
        Amnesty imesema kuwa ‘’uongozi wa rais Samia Suluhu Hassan umeleta matumaini ya uhuru wa kujieleza, lakini vitendo vya hivi karibuni vya kukamatwa kwa wanachama wa vyama vya upinzani vinatia wasiwasi kama uhuru huu utaendelea ama hali itarudi kama ilivyokua awali’’.
Polisi nchini Tanzania imesisitiza kuwa Mbowe amefanya makosa na ushahidi upo.
‘’Wafuasi wa CHADEMA wanadhani Mbowe ameonewa na kuwa yeye ni malaika hawezi kufanya makosa, lakini kesi hii iko mahakamani  hivyo tuachie mahakama ifanye kazi yake na ukweli utajulikana’’ alisema IGP Simon Sirro mkuu wa polisi Tanzania.
Mbowe alikamatwa wiki mbili zilizopita na baadae kusomewa mashtaka ikiwemo ugaidi.



No comments

Powered by Blogger.