Afisa wa polisi wa trafiki anauguza majeraha kwenye uso wake baada ya kushambuliwa na raia alipokuwa kazini. Kisa hicho kimefanyika Jumapili Novemba 7,2021 katika mzunguko wa magari eneo la Kariokor jijini Nairobi nchini Kenya ambapo Afisa huyo alikuwa akisaidia kuelekeza magari wakati jamaa mmoja aliibuka ghafla na kumtwanga ngumi usoni. Kutokana na ngumi hiyo nzito aliyopigwa na mhuni huyo, Askari poli alishikwa na kizunguzungu na kuanguka huku akivunja damu na ndipo Msamaria Mwema akamkimbiza hospitali
No comments
Post a Comment