Header Ads

Header ADS

Ethiopia yazuia msaada kwa waathiliwa wa ubakaji

     Katika ripoti  mpya ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch imeishutumu serikali ya Ethiopia kwa kuzuia misaada kwa vituo vya afya na kuzuia waathiriwa wa ubakaji kupata msaada.
Ripoti hiyo yenye kurasa 89 ina maelezo ya athari za kiafya na unyanyapaa wanaokumbanao waathirika wa ubakaji wenye umri wa miaka sita hadi 80 tangu kuanza kwa vita vya kivita huko Tigray mwezi Novemba mwaka jana.
Serikali ya Ethiopia hapo awali ilikana kuzuia kwa makusudi misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.

HRW inashutumu pande zinazozozana kufanya unyanyasaji wa kijinsia ulioenea huku zikilenga vituo vya afya makusudi, na kuwaacha waathirika na jamii zao kushindwa kupata matibabu.
Inafafanua majeraha ya kimwili na kisaikolojia yanayotokea, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya zinaa, mifupa iliyovunjika, majeraha ya kuchomwa, fistula na maradhi ya msongo wa mawazo.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu linasema Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na wafadhili wa kimataifa wanapaswa kuishinikiza serikali ya Ethiopia na pande zote zinazohusika katika mzozo huo kusitisha dhuluma na kuruhusu uchunguzi wa kimataifa kuhusu madai ya unyanyasaji huo.


No comments

Powered by Blogger.