Malawi ya weka historia ya kwanza kuwa na Mbunge Mualbino
Mmalawi wa kwanza mwenye ualbino aliyechaguliwa kuwa mbunge amechukua kiti chake katika bunge jipya siku ya Jumatatu, na kuweka historia katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Overstone Kondowe, mwenye umri wa miaka 42 alikulia kijijini bila msaada wowote wa kupunguza maumivu katika ngozi yake isiyo na jua au miwani ili kusaidia macho yake duni.
Ualbino unanyanyapaliwa na kuzungukwa na ushirikina hivi kwamba watu walio na hali hiyo wanaishi katika hatari ya kila siku kutokana na mashambulizi ya nasibu na biashara ya mauaji ya viungo vya mwili, vinavyotumiwa katika uchawi.
Watoto wengi hawaendi shule. Lakini Kondowe, ambaye alianza kuhudumu wadhifa wake mpya Bungeni siku ya Jumatatu, anatumai kuchaguliwa kwake kumeweka historia katika nchi ambayo watu 134,636 wanaishi na ualbino.
"Hii ni ishara kubwa kwamba Wamalawi wanatukubali," alisema.
Aliendela kusema: "Inanipa ujasiri kwamba ninaweza kufikia mambo makubwa zaidi maishani na kwamba watu wanaweza kuniamini.
"Nchi ya Malawi na nchi jirani ya Tanzania zina historia ndefu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kuuawa kwa ajili ya viungo vyao vya mwili, kutumika katika matambiko, uchawi na inaaminika kuleta bahati nzuri.
Kondowe, rais wa zamani wa Chama cha Watu Wenye Ualbino nchini Malawi (APAM), amesema ingawa mashambulizi ya viungo vya mwili yamepungua, kutokana na mashitaka machache ya hali ya juu, bado kuna njia ndefu ya kufanya na mipango ya kufanyia kazi sheria ya kuwalinda watu wote wenye ulemavu.

No comments
Post a Comment