Jaji Joachim Tiganga aahirisha kesi inayowakabili akina Mbowe na wenzake watatu
Jaji Joachim Tiganga leo Jumatano Novemba 17, 2021 ameahirisha mara tatu kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu kwa sababu tofauti ikiwemo kuruhusu mawakili wa pande zote kujadiliana.
Awali Jaji Tiganga aliahirisha kesi hiyo kwa muda kwa ajili ya kwenda kukagua kilichomo kwenye diary aliyokutwa nayo shahidi wa Jamhuri kizimbani.
Mara ya pili Jaji alilazimika kuahirisha kesi hiyo ili kuruhusu majadiliano na mawakili wa pande zote juu ya maudhui waliyoyaona kwenye diary hiyo.
Hata hivyo, kesi hiyo itaendelea baada ya majadiliano ya tatu kukamilika
No comments
Post a Comment