Israel imefanya mashambulizi ya makombora kusini mwa Syria
Israel imefanya mashambulizi ya makombora mapema leo kusini mwa Syria.Hayo yameripotiwa na shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Syria, SANA.SANA imesema makombora hayo yalifyatuliwa kutoka milima ya Gholan na yalilenga jengo lililokuwa kusini mwa Damascus.
Hata hivyo mashambulizi hayo hayakusababisha vifo kwa kuwa hakukuwa na watu ndani ya jengo hilo.Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ya aina hiyo na nchini Syria mara kwa mara ikidai inalenga kambi za wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran mfano wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon.
No comments
Post a Comment