Header Ads

Header ADS

Mbadala wa Miquissone

 Kocha msaidizi wa kikosi cha Simba, Hitimana Thierry amethibitisha kuwa mshambuliaji wake mpya Pape Ousmane Sakho amerejea kikosini baada ya kupona maumivu ya mguu yaliyokuwa yanamkabiri mwezi mmoja uliopita.

Hitimana ameanza kwa kusema, "Sakho ni mchezaji ambaye ana faida mbili, anaweza kucheza kama kiungo lakini pia kama mshambuliaji wa pili, urejeo wake ni mzuri katika timu na mwalimu mkuu ndiyo atajua kama atamtumia katika mchezo ujao au vipi”.

Ikumbukwe kuwa, Sakho aliumia kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ambapo alicheza madhambi dakika 12 za mwanzoni miezi miwili iliyopita na kukosa michezo 5, dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Jwaneng Galaxy, Namungo na michezo miwili ya Jwaneng Galaxy ya mtoano klabu bingwa Afrika.

Kwa upande wa maandalizi ya Simba kwenye michezo ijayo amesema bado wanaelekeza nguvu kwenye michezo yake miwili ya mtoano dhidi ya Red Arrows ya Zambia kuwania kufuzu makundi kombe la Shirikisho Afrika.

"Tuna mechi za ligi kuu kwa kipindi hiki lakini pia tuna mchezo muhimu wa hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho Afrika hivyo tunapokuwa na kundi kubwa la wachezaji waliofiti inatuweka katika hali nzuri kwenye maandalizi yetu" Hitimana amesema.

Simba inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting na kisha kucheza mchezo wake wa mtoano wa mwisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia kuwania kufuzu Makundi michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 11, baada ya kucheza michezo 5 ilhali Maafande wa Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama 6.



No comments

Powered by Blogger.