Header Ads

Header ADS

Mahakama yatupa pingamizi kesi kina Mbowe

 Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Akisoma uamuzi huo leo Jumatatu Novemba 15, 2021 Jaji Joachim Tiganga amekubaliana na hoja za upande wa mashitaka na kukubali barua iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama itolewe kama kielezo na Shahidi namba mbili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Mawakili upande wa utetezi walipinga kuhusiana na barua ambayo upande wa mashtaka uliomba kuiwasilisha mahakamani kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo.

Upande wa mashtaka Ijumaa iliyopita kupitia kwa shahidi huyo wa pili uliiomba mahakama iipokee barua hiyo ya msajili inayoonesha kuwa upande wa mashtaka umeomba kitabu cha kumbukumbu za Mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam cha mwaka 2020, ili shahidi huyo aweze kukiwasilisha mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wake na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.



No comments

Powered by Blogger.