Header Ads

Header ADS

Tasaf yatenga Sh24.3 bilioni kutekeleza miradi Mkoani Njombe

 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (Tasaf) imetenga Sh24.3 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya awamu ya nne ya kupunguza umasikini mkoani Njombe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga amesema hayo wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani humo kuwa fedha hizo zitasaidia kupunguza changangamoto zilizopo za miundo mbinu.

Amesisitiza kufuata utaratibu wa kisheria katika matumizi ya fedha hizo.

"Kitu kikubwa  kuhakikisha kwamba tunatekeleza miradi ambayo ndiyo uhitaji halisi wa  wananchi katika maeneo yao" amesema Mwamanga.

Mkuu wa mkoa wa Njombe,  Mhandisi Marwa Rubirya amewataka wataalam na wasimamizi wa miradi hiyo kufuata weledi na uadilifu katika majukumu yao.

Amesema uongozi wa mkoa na wilaya hautawavumilia watendaji ambao watajihusisha na vitendo vya kuhujumu miradi hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Meneja miradi wa Tasaf, Paul Kijazi amesema katika miradi iliyopita yapo mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya na elimu hasa katika ujenzi wa madarasa na vituo vya afya na zahanati.



No comments

Powered by Blogger.