Header Ads

Header ADS

Nchi masikini kuchangiwa na Ujerumani

 Ujerumani itachangia euro milioni 150 za ziada kuzisaidia nchi maskini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. 

Wizara za Ujerumani za Mazingira na Maendeleo zimetangaza hayo jana ikiwa ni wiki ya pili ya mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi COP26, unaofanyika mjini Glasgow, Scotland. 
 
Mchango huo ni sehemu ya fedha za umma ambazo Ujerumani inatoa kila mwaka kwa nchi maskini kuzisaidia kujilinda dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

 


No comments

Powered by Blogger.