Waasi wavamia vijiji vya Chanzu,Runyoni, wakazi wakimbia makazi yao DRC
Kundi lisilojulikana lenye silaha limeshambulia vijiji vya mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini mwa DR Congo karibu na mpaka na Uganda na kusababisha mamia ya raia kuyaacha makazi yao.
Wenyeji wanasema kuwa washambuliaji waliwakimbiza idadi ndogo ya jeshi la taifa ili kukalia Chanzu, Runyoni, Ndiza, na vijiji zaidi katika eneo la Rutshuru.
Shirika la kiraia huko Rutshuru linashuku waasi wa M23 ambalo mnamo 2013 lilitia saini makubaliano na serikali ya kuwaondoa na kumaliza uasi, halijasema chochote kuhusu shambulio hilo.
Mamia wamefunga mpaka wa Bunagana wa nchi hiyo na Uganda asubuhi ya leo'', Bw. Ayobangira Safari mbunge wa mkoa huo ameiambia BBC Idhaa ya maziwa makuu.
Vijiji vilivyoshambuliwa "vilikuwa ngome ya waasi wa M23 kabla ya kushindwa vita na jeshi " na kuhamishwa, mbunge huyo alisema.
Wiki iliyopita waasi walishambulia na kuudhibiti mji wa Bukavu Kusini kwa saa kadhaa.
No comments
Post a Comment