Header Ads

Header ADS

Serikali yawataka wataalamu wa elimu kutoa elimu sahihi ili kuboresha elimu

     Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde  wakati akiongea na   Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa taarifa na takwimu sahihi za elimu ili kuboresha usimamizi  wa  elimu

    Mhe . David Silinde  ameyasema hayo   Jijini  Arusha wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Nane wa  Umoja wa Maafisaelimu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara(REDEOA) lengo likiwa ni kujifunza, kubadilishana uzoefu na namna ya  kuzitatua changamoto katika utendaji kazi wa shughuli za kielimu.

Katika mkutano huo Mhe. Silinde amewataka viongozi hao kusimamia miradi ya elimu na  kuwepo na  taarifa na takwimu sahihi za kielimu ili  elimu inayotolewa iendane na  uhitaji wa sehemu husika.  Aidha, amewaelekeza viongozi hao kuzitatua changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu.

Amesisitiza kusimamia suala la uandikishaji kwa wanafunzi wa darasa Awali na Kwanza Mhe. Silinde amesema bado ni changamoto amezielekeza  Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwemo wasimamizi wa elimu kuhakikisha wanasimamia suala la uandikishwaji  wa  wanafunzi  ili  watoto  wapate  elimu.  “Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu imeidhinisha fedha kiasi cha shilingi bilion 304  kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu  ya  kufundishia  na kujifunzia amesema ni vyema watoto  wapate elimu ili Taifa liwe na wataalam wengi na bora.

Vilevile ameeleza kuhusu azma ya Serikali ya  kuendelea kuajiri  walimu  na kuendelea kuboresha maslahi yao amewataka wasimamizi  hao  kufanya  kazi kwa waledi  katika utoaji na kusimamia  walimu. Akizungumzia   ununuzi wa magari ya Maafisaelimu Sekondari amesema magari hayo yameshaagizwa  na taratibu zitakapokamilika hivi karibuni watakabidhiwa   amesema  hayo yote ni katika kuboresha sekta ya elimu ili waweze kusimamia.

 “Nimeridhishwa na kauli mbiu hii ya   “Kuboresha Miundombinu ya Shule ni Kuimarisha Elimu kwa Maendeleo endelevu na Kukuza Uchumi wa Taifa” kauli mbiu inaendana  na malengo na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa adhma yake ni kuhakikisha, kuendeleza elimu bila malipo na kuboresha miundombinu ya elimu”. amesema  Mhe. Silinde

Aidha, nitoe msisitizo kwa wasimamizi wa elimu kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wanahudhuria darasani kila siku kulingana na ratiba za masomo zilivyopangwa ili kuepuka kuathiri utekelezaji wa Kalenda za mtaala.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe  akitumia mkutano huo kwa kuwapongeza maafisa hao kwa usimamizi wa madarasa 15000 ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO – 19,  na kuwaelekeza Wakurugenzi kuendelea na  usimamizi wa fedha za Serikali  na kupanga bajeti vizuri ya fedha za mapato ya ndani ili kujenga  na kuendeleza ujenzi wa matundu ya vyoo  mashuleni.

Kwa upande wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amewahakikishia watumishi wote wa Umma kuwa, usimamizi wa haki za watumishi utaendelea kwa kuzingatiwa  Sheria, Taratibu za Utumishi wa  Umma na kuelezea mfumo wa uhamisho kwa walimu na watumishi unafanyiwa kazi hivi karibu utakuwa tayari kutumika na kabla ya kutumika kutakuwa na mafunzo ili kuwe na uwelewa katika kuufanyia kazi katika kutenda haki  amesema hii itasaidia mgawanyo sawa kwa watumishi sehemu za kazi.

  



No comments

Powered by Blogger.