Header Ads

Header ADS

Katibu wa Baraza la Walei auawa ndani ya eneo la Kanisa Katoliki, kichwa chatenganishwa na kiwiliwili

Nickson Myamba ambaye ni katibu wa baraza la walei kigango cha Makambako, jimbo la Njombe, amekutwa ameuawa kwa kutenganishwa kichwa na mwili wake ndani ya Kanisa Kuu Katoliki la Parokia ya Makambako usiku wa Februari 7, 2022.

Mauaji hayo ya kutisha ambayo siyo ya kawaida kuwahi kutokea katika maisha ya kanisa hilo la Mtakatifu Bikira Maria Mama wa Neema, ambapo marehemu aliuawa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

Akizungumza katika misa ya mazishi ya kiongozi huyo wa kanisa aliyeuawa ndani ya duka la vitabu vya imani, Padre Jordani Mwajombe, Decanusi wa Makambako amewataka waumini kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi.




No comments

Powered by Blogger.