Polisi wataka wananchi kujitokeza Mahakamani kutoa ushahidi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo, amewataka wananchi kujitokeza mahakamani kutoa ushahidi ili kuepukana na changamoto ya kesi nyingi kuharibika kutokana na ushahidi kukosekana, kitendo ambacho kinapelekea watuhumiwa wanaokamatwa kuendelea kutamba mtaani.
Kauli hiyo ameitoa wakati akipokea kituo kidogo cha polisi Kisongo kilichojengwa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa IRMCT Arusha, na kusema kwamba upo umuhimu wa watu kufika mahakamani pale wanapohitajika
No comments
Post a Comment