wizara ya ulinzi Ukraine yalipua daraja kuzuia wanajeshi wa Russia kuingia katika mji wa kyiv
Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema imelipua daraja la mto wa Teteriv liliopo kaskazini mwa mji wa Kyiv kwa jitihada za kuzuia wanajeshi wa Russia kuvamia eneo hilo
Katika taarifa yake wizara hiyo imesema wameweza kuzuia majeshi ya Russia kuendelea kuingia kwa kutumia mpaka wa Belarus uliopo umbali wa kilometa 32 kufikia mji mkuu.
Soma zaidi: Zaidi ya wanajeshi 40 wauawa Ukraine, mataifa yalaani
Wakati taarifa za kuongezeka kwa idadi ya watu waliofariki baada ya Russia kuivamia Ukraine leo, viongozi mbalimbali duniani wametoa matamko ya kulaani uvamizi huo wakitaka usitishwe mara moja.
Karibu watu 18 na wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Russia leo Alhamisi Februari 24, 2022 asubuhi katika mji wa Odessa ulio pwani ya Black Sea, serikali imesema.
No comments
Post a Comment