Rais , Samia akataa tabia ya kutukuzwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemuahidi Askofu Severine Niwemugizi, kwamba yeye si mtu wa kutaka kutukuzwa na mara nyingi amekuwa akijitahidi kujishusha ili awe sawa na wengine.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 22, 2022, wakati akishiriki Jubilee ya miaka 25 ya utumishi wa kiaskofu wa Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge, Ngara
mkoani Kagera
"Baba Askofu umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hiyo si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine, maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie, na sio nijitukuze kwenu," amesema Rais Samia
No comments
Post a Comment