Waandishi wa habari wawili wakamatwa na maafisa wa kundi la Taliban
Waandishi wawili wa habari wanaofanya kazi na kituo binafsi cha televisheni nchini Afghanistan wamekamatwa na maafisa wa kundi la Taliban kwenye mji mkuu Kabul kwa sababu ambazo hazijulikani. Wafanyakazi wenzao wa kituo maarufu cha televisheni cha Ariana wamesema Waris Hasrat na Aslam Hijab walikamatwa jana na maafisa walio na silaha mbele ya jengo la ofisi za kituo hicho.
Familia za waandishi hao zimetoa wito kwa makundi ya kutoa msaada kwa waandishi wa habari pamoja na waandishi wengine kupaza sauti ili kusaidia kuachiwa huru kwa wawili hao ambao hata hivyo serikali ya Taliban inakanusha kuwashikilia.
Kukamatwa kwao kumetokea siku moja baada ya mgeni aliyealikwa kwenye mdahalo unaorushwa na kituo cha Ariana kuukosoa utawala wa Taliban ambao umechukua hatamu za uongozi nchini Afghanistan tangu mwezi Agosti mwaka jana.
No comments
Post a Comment