Header Ads

Header ADS

Nchi ya Ethiopia ya hofu kuongezeka kwa vita katika mji wa oromia

 Kuendelea kwa mapigano katika eneo lenye watu wengi zaidi nchini Ethiopia, Oromia, kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Oromo Liberation Army (OLA) kunazua wasiwasi wa kuzorota kwa ukosefu wa usalama katika eneo la kusini.
Mamlaka huko Oromia wanasema wameanzisha mashambulizi ya mwezi mzima dhidi ya OLA, lakini kundi la waasi linasema kuwa linashinda vita.







Msemaji wa OLA Odaa Tarbii alitweet kwamba vikosi vya usalama kutoka eneo jirani la Somalia vimetumwa Oromia kutoa msaada katika mapigano.

Lakini akizungumza na BBC, Abfikadr Rashid, afisa mkuu wa eneo la Somalia, alikanusha madai hayo lakini akasema vikosi kutoka eneo lake vinaweza kuingia Oromia ikiwa wataalikwa.

Kuna hofu kwamba kuongezeka kwa mapigano kusini mwa nchi kunaweza kuzidisha machafuko ya kisiasa na kibinadamu ambayo nchi hiyo inakabiliwa nayo.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 17, Kaskazini mwa Ethiopia, vimezua mzozo mkubwa wa kibinadamu ambapo maelfu ya watu wameuawa na mamilioni kuachwa wakihitaji msaada.

Makubaliano ya kibinadamu yaliyokubaliwa kati ya vikosi vya Tigrayan na serikali mwezi uliopita yalionekana kama hatua muhimu ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mwa nchi hiyo.

Lakini kiasi cha usaidizi unaotolewa kwa Tigray hakitoshi kukidhi mahitaji katika eneo hilo, huku kukiwa na shutuma kwamba msaada unazuiliwa.

No comments

Powered by Blogger.